array(0) { } Radio Maisha | Pigo kwa Serikali baaya mahakama kukosa kutoa uamuzi kuhusu asilimia 1.5

Pigo kwa Serikali baaya mahakama kukosa kutoa uamuzi kuhusu asilimia 1.5

Pigo kwa Serikali baaya mahakama kukosa kutoa uamuzi kuhusu asilimia 1.5

Kwa mara nyingine, serikali imepata pigo baada ya Mahakama ya Juu kukosa kutoa uamuzi kuhusu ombi la kutaka wafanyakazi kuanza kutozwa asilimia 1.5 ya mishahara yao ili kugharimia ujenzi wa makazi ya bei nafuu.

Jaji Maureen Onyango amesema uamuzi huo utatolewa tarehe 27 mwezi huu huku serikali ikitakiwa kushauriana na washikadau wengine kabla kutekelezwa kwa agizo hilo.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Shirika la Watumiaji wa Bidhaa, COFECK, Shirikisho la Waajiri, FKE na Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi, COTU.

Kupitia matozo hayo, serikali inalenga kukusanya shilingi bilioni 57 kila mwaka ili kufanikisha ujenzi wa nyumba laki tano katika muhula huu wa mwisho wa Rais Uhuru Kenyatta.