array(0) { } Radio Maisha | Kaunti nne za Pwani kufaidi na ufadhii wa Benki ya Dunia.

Kaunti nne za Pwani kufaidi na ufadhii wa Benki ya Dunia.

Kaunti nne za Pwani kufaidi na ufadhii wa Benki ya Dunia.

Benki ya Dunia imetoa ufadhili wa mabilioni ya fedha kuzisaidia kaunti nne za Pwani; Mombasa, Kwale, Taita Taveta na Kilifi katika utekelezaji wa miradi ya maji kwenye hafla ambayo imeongozwa na Naibu wa Rais William Ruto.

Akizungumza wakati wa kutiwa saini mkataba huo, Ruto amesema ufadhili huu unalenga kuboresha si sekta ya maji pekee bali pia elimu na miundo msingi.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Simon Chelugui amewashauri magavana kutumia fedha hizo kwa miradi ambayo imetengewa. Chelugui amesema utekelezaji wa miradi hiyo itaanzia Kaunti ya Taita Taveta.

Magavana wa kaunti hizo nne wameipongeza serikali na benki hiyo kufuatia ufadhili huo huku wakiahidi kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa. Granton Samboja ni Gavana wa Taita Taveta.

Kaunti ya Mombasa imepata shilingi bilioni tatu, Kwale shilingi bilioni 2.5, Taita Taveta bilioni 2.5 , huku Kilifi ikipata shilingi bilioni 2.7.