array(0) { } Radio Maisha | Cleopas Malala Rashid Echesa,Justus Murunga na Libinus Oduor kuripoti katika idara ya polisi

Cleopas Malala Rashid Echesa,Justus Murunga na Libinus Oduor kuripoti katika idara ya polisi

Cleopas Malala Rashid Echesa,Justus Murunga na Libinus Oduor kuripoti katika idara ya polisi

Seneta wa Kakamega Cleopas Malala, aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa, Mbunge wa Matungu Justus Murunga na Mwakilishi wa Wadi ya Mayoni Libinus Oduor wanatarajiwa kuripoti katika idara ya polisi wakati wowote kuanzia sasa kwa kuhusishwa na mauaji ya Matungu Kaunti ya Kakamega.

Viongozi hao watajiwasilisha kufuatia agizo la Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Noordin Hajji la kuwataka kufika katika Idara ya Upelelezi baada ya kuachiliwa jana kwenye vituo mbalimbali vya polisi.

Kabla ya kuachiliwa huru, wafuasi wa Seneta Malala ambaye alikuwa amezuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kisumu walizua rabsha kituoni humo wakishinikiza kuachiliwa kwake na hivyo kuwalazimu polisi kufyetua vitoza-machozi hewani kuwatawanya.

Baada ya kuachiliwa, Malala alisema atawashtaki Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Fred Matiang'i na Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai kufuatia kukamatwa kwake na kuzuiliwa kwa kipindi cha siku mbili bila ya kuelezwa sababu.