array(0) { } Radio Maisha | Misa ya wafu ya Justin Bundi inatarajiwa kufanyikaJumatatu

Misa ya wafu ya Justin Bundi inatarajiwa kufanyikaJumatatu

Misa ya wafu ya Justin Bundi inatarajiwa kufanyikaJumatatu

Misa ya wafu ya aliyekuwa Karani wa Bunge la Kitaifa Justin Bundi inatarajiwa kufanyika Jumatatu. Misa hiyo itafanyika katika Kanisa Katoliki la Don Bosco, Upper Hill, Nairobi huku mipango ya mazishi ikiendelea.

Bundi alifariki dunia wiki iliyopita  alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Agha Khan akiugua saratani.

Viongozi mbalimbali walituma risala za rambirambi kwa familia na jamaa za mwendazake huku Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi akimtaja Bundi kuwa kiongozi aliyeifanya kazi yake kwa uadilifu na kwamba atakumbukwa kwa kuwa muasisi mkubwa wa mabadiliko makuu katika bunge. 

Bundi alistaafu mwaka 2017, huku nafasi yake ikichukuliwa na Michel Sialai. Marehemu Bundi aliwahi kuwa Karani wa Bunge la Afrika Mashariki.