array(0) { } Radio Maisha | Sossion arejelea wito wake wa kuwata Walimu kusitisha mafunzo ya Mtalaa wa Umilisi.

Sossion arejelea wito wake wa kuwata Walimu kusitisha mafunzo ya Mtalaa wa Umilisi.

Sossion arejelea wito wake wa kuwata Walimu kusitisha mafunzo ya Mtalaa wa Umilisi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT Wilson Sossion arejelea wito wake kwa walimu kusitisha mafunzo ya Mtalaa wa Umilisi, CBC na badala yake kutoa mafunzo kuhusu mtalaa wa kale 8-4-4.

Akizungumza kwenye eneo la Koibatek, Sossion amesema washikadau wote hawakuhusishwa katika harakati za kuutekeleza mtalaa huo mpya.

Sossion amemsuta Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha kwa kutumia nguvu kuutekeleza mtalaa huo, badala ya kuhakikisha miundo msingi katika sekta hiyo inaboreshwa.

Haya yakijiri huku Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi amemshauri Magoha kutowapuuza washikadau wengine katika sekta hiyo. Mudavadi ameonya kwamba huenda sekta hiyo ikadorora iwapo viongozi wengine hawatahusishwa.

Kauli yake imetiliwa mkazo na Seneta wa Homa Bay, Moses Kajwang ambaye amemtaka Magoha na Sossion kuweka kando tofauti zao ili kufaulisha mtalaa huo.