array(0) { } Radio Maisha | Naibu wa Rais William Ruto aendelea kupigiwa Kampeni na Wandani wake.

Naibu wa Rais William Ruto aendelea kupigiwa Kampeni na Wandani wake.

Naibu wa Rais William Ruto aendelea kupigiwa Kampeni na Wandani wake.

Viongozi wa kisiasa wanaendelea kupiga ngoma ya mwaka wa 2022 huku wandani wa Naibu wa Rais William Ruto sasa wakimmiminia sifa na kumtaja kuwa kiongozi tosha kuutwaa uongozi wa taifa hili wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa amesema Ruto amekuwa akiwahudumia wakenya bila kujali kabila, dini wala vyama vya kisiasa.

Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa aidha amewashauri wananchi kumchagua Ruto iwapo wangependa taifa hili lisonge mbele kimaendeleo huku akimsuta Kinara wa ODM, Raila Odinga kwa madai kwamba kudorora kwa uchumi nchini unatokana na vitendo vyake.

Hata hivyo, kundi linalomuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta limewasuta wandani wa Ruto wakiwataka kukoma kuendesha siasa za mwaka wa 2022. Ngunjiri Wambugu ni Mbunge wa Nyeri Mjini.