array(0) { } Radio Maisha | Familia ya Seneta, Malala inataka aachiliwe ikidai yu mgonjwa

Familia ya Seneta, Malala inataka aachiliwe ikidai yu mgonjwa

Familia ya Seneta, Malala inataka aachiliwe ikidai yu mgonjwa

Familia ya Seneta wa Kakamega Cleophas Malala,  imelalamikia hali yake tangu alipokamatwa na kuzuiliwa korokoroni hapo jana.  Kulingana na jamaa zake,  seneta huyo ambaye anahusishwa na mauaji ya Matungu hajaruhusiwa kuwaona madaktari wake wala mawakli.   Aidha wanadai kwamba  hajapewa chakula wala maji safi ya kunywa.

Wakili wake Charles Malala, amesema seneta huyo anaugua kisukari pamoja na shinikizo la damu na anahitaji dawa ambazo hajazitumia tangu alipokamatwa .

Hayo yanajiri huku wazazi wake wakimtetea dhidi ya madai hayo, huku babake David Malala akisema ana uhakika mwanawe hajatekeleza mauaji hayo.

Wafuasi wake idha  wamekita kambi nje ya kituo cha Polisi anakozuiliwa wakitaka aachiliwe. Seneta Malala atasalia korokoroni Wikendi Nzima hadi Jumatatu atakapofikishwa mahakamani.