array(0) { } Radio Maisha | Mbunge wa Matungu amekamatwa, kufuatia mauaji eneo hilo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mbunge wa Matungu amekamatwa, kufuatia mauaji eneo hilo

Mbunge wa Matungu amekamatwa, kufuatia mauaji eneo hilo

Hatiyame Mbunge wa Matungu, Justus Murunga amekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji yanayoendelezwa katika eneo la Matungu, Kaunti ya Kakamega. Maafisa wa usalama walikuwa wamemtaka mbunge huyo kujisalimisha hapo jana.  Alikuwa miongoni mwa wanasiasa waliohudhuria mkutano mmoja katika eneo la Ikolomani japo inaarifiwa aliondoka kwa haraka baada ya mkutano huo kukamilika.

 Aidhha maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI usiku wa kuamkia leo walifanikiwa kumkamata mshukiwa mwingine jijini Nairobi na kumsafirishwa hadi katika Kaunti ya Vihiga.

Hayo yanajiri huku Seneta wa Kakamega, Cleophas Malala, aliyekuwa Waziri wa Michezo, Rashid Echesa na Mwakilishi Wadi wa eneo la Mayoni, Libinus Oduori wakitarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu baada ya kukamatwa jana na maafisa wa Idara ya Upelelezi kwa kuhusishwa na mauaji hayo. Kamanda wa Polisi katika eneo la Nyanza, Vincent Makokha alisema Malala atazuiliwa korokoroni hadi siku ya Jumatatu wakati atakapowasilishwa mahakamani.

Echesa kwa  upande wake alihojiwa na polisi katika eneo la Kakamega na baadaye usiku kupelekwa eneo lisilo julikana huku pia akitarajiwa kuwasilishwa mahakamani Juamatatu. Vurugu zilishuhudiwa baina ya maafisa wa usalama na Malala wakati alipotaka kuelezwa sababu za kukamatwa kwake.

Hatua dhidi ya wanasiasa hao zilianza kuchukuliwa baada ya Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i siku ya Alhamisi kuzindua oparesheni ya usalama katika eneo la Matungu na kuonya kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiyafadhili makundi ya vijana kutekeleza mavamizi. Kufikia sasa, watu kadhaa wameuliwa na wanaoaminika kuwa wanachama wa kundi linalojiita 42 Brothers.

Wakazi wa eneo hilo wameelezea kuunga mkono hatua ambazo zimechukuliwa kufikia sasa dhidi ya wanasiasa wanaodaiwa kuchochea mauaji.