array(0) { } Radio Maisha | Wanafunzi wa Peter Tabichi watuzwa Marekani

Wanafunzi wa Peter Tabichi watuzwa Marekani

Wanafunzi wa Peter Tabichi watuzwa Marekani

Mwalimu Mkenya aliyeshinda tuzo ya kuwa mwalimu bora duniani Peter Tabichi, ana sababu nyingine ya kutabasamu baada ya wanafunzi wake wawili kutuzwa shilingi laki mbili katika shindano la Sayansi Nchini Marekani.

Wanafunzi hao Esther Amimo Anyanzwa na Salome Njeri kutoka Shule ya Upili ya Mseto ya Keriko mjini Nakuru wametuzwa tuzo la UN Sustainable Development Goal Award.

Wawili hao walizindua mashine itakayowasaidia wanafunzi wasio na uwezo wa kuona na kusikia.

Wawili hao ni miongoni mwa wanafunzi 10 walio wakilisha Kenya katika eneo la Phoenix Arizona.