array(0) { } Radio Maisha | HUDUMA NAMBA:Wakenya wajitokeza kwa wingi kusajiliwa wakati wa mwisho

HUDUMA NAMBA:Wakenya wajitokeza kwa wingi kusajiliwa wakati wa mwisho

HUDUMA NAMBA:Wakenya wajitokeza kwa wingi kusajiliwa wakati wa mwisho

Zikiwa zimesalia saa chache tu kabla ya muda wa kusajiliwa kwa watu kupata Huduma Namba kukamilika Waziri wa Usalama na Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiangi, amesema kufikia sasa idadi kubwa wamesajiliwa huku akisema huenda idadi ikafikisa milioni thelathini na tano.

Akizungumza jijini Nairobi Matiangi  hata hivyo amesikitikia idadi kubwa ya watu ambao wamejitokeza wakati wa mwisho kusajiliwa.

Amesisitiza kwamba shughuli yenyewe itakamilika hapo kesho kwani hakuna fedha za kutosha kuongeza muda wa usajili huo, huku akiwahakikishia wale wote ambao wamefika vituoni kusajiliwa kuwa watahudumiwa. Waziri huyo amesema ripoti kuhusu usajili wenyewe itawasilishwa kesho kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Ikumbukwe siku arubani na nne zilizopita serikali ilizindua mpango wa usajili wa watu hatua ambayo imesisitiza kuwa itarahisha utoaji huduma kwa njia ya dijitali.