array(0) { } Radio Maisha | KISWAHILI KITUKUZWE:Kenya imetia saini kuanzisha somo la Kiswahili Afrika Kusini

KISWAHILI KITUKUZWE:Kenya imetia saini kuanzisha somo la Kiswahili Afrika Kusini

KISWAHILI KITUKUZWE:Kenya imetia saini kuanzisha somo la Kiswahili Afrika Kusini

Serikali ya Kenya imetia saini mkataba na ile ya Afrika Kusini kufuatia hatua ya taifa hilo kuanzisha Somo la Kiswahili nchini humo. Waziri wa Elimu wa Kenya Profesa George Magoha na Mwenzake wa Afrika Kusini, Angelina Matsie Motshekga wamesema mkataba huo utahakikisha kuwa Kenya inaisaidia Afrika Kusini kufanikisha hatua hiyo kukiwamo kuwatuma walimu wa Kiswahili. Aidha wamesema ushirikiano huo utaimarisha uhusiano wa raia wa mataifa haya mawili.

Waziri Motshekga amesema kuna idadi kubwa ya raia hasa wa Kenya wanaotafuta mafunzo Afrika Kusini ambao huzungumza lugha ya Kiswahili hivyo kuna haja ya kuimarisha uzungumzaji wa lugha hiyo nchini humo.

Mbali na Kiswahili Kenya inatarajiwa kushirikiana na Afrika Kusini kuimarisha mafunzo kupitia mfumo wa dijitali.