array(0) { } Radio Maisha | Pigo kwa Vyuo Vikuu Nchini kufuatia uhaba wa fedha

Pigo kwa Vyuo Vikuu Nchini kufuatia uhaba wa fedha

Pigo kwa Vyuo Vikuu Nchini kufuatia uhaba wa fedha

Vyuo vikuu vya umma nchini vinakabiliwa na uhaba wa fedha za kutekeleza majukumu yake huku serikali ikisisitiza haitaziongeza fedha. Wakuu wa vyuo wamelalamikia idadi ndogo ya wanafunzi wa kujilipia  wanaojiunga na vyuo vikuu baada ya serikali kuongeza iddai ya wale wanaoafadhiliwa na serikali kwa kushusha alama za wanaoweza kujiunga na vyuo vikuu hadi C+.

Kwa muda sasa vyuo vikuu vinekuwa vikitegemea wanafunzi wa kujilipia ambao ada zao za karo  huwa juu na kufifikia takriban laki moja kwa mwaka huku wale wanaofadhiliwa na serikali wakilipa shilingi elfu 30 kwa mwaka. Kuanzia mwaka 2017 serikali imeendelea kuongeza idadi ya wanafunzi wa serikali na kuathiri  hali ya kifedha ya vyuo.  Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi Prof Mbithi katika mahojiano ya awali aliwahi kuelezea kwa kina changamoto hii.

Hali hii ya Kenya kutegemea wanafunzi wa kujilipia  ni tofauti na Vyuo Vikuu vya Kimatiafa ambavyo kando na kupata mgao wa kutosha wa serikali, pia hupata ufadhili kutoka kwa wanafunzi wa zamani na mashirika ya kufadhili utafiti.

Katika mkutano uliofanyika hivi karibuni kati  ya vyuo na Waziri wa Elimu Prof George Magoha, ilibanika kwamba vyuo vina deni la hadi shilingi bilioni 18 za matozo ya wafanyakazi wake kwa Mamlaka ya Utozaji Kodi na hazina nyingine muhimu.

Ili kukabili hali hiyo sasa Waziri Magoha badala ya kuongeza ufadhili wa serikali amewataka wakuu hao kuanza kuwafuta kazi baadhi ya wafanyakazi katika vyuo.

Kadhalika baadhi ya idara huenda zikajumuishwa. Vyuo vya binafsi ambavyo vilevile vilianza kuwachukua wanafunzi wanaofadhiliw ana serikali pia vinalalamikia kiwango kidogo kinachotumwa na serikali kwa fadhili wao. Hata hivyo, Waziri Magoha amevitaka kuwaachilia zaidi ya wanafunzi elfu 40 wa serikali iwpao haviridhiki na mgao wanaopewa. Kinaya cha serikali kuongeza idadi ya wanaofuzu vyuoni ni hali ya ukosefu wa ajira nchini huku kiwango kikubwa cha ajira kikiwa katika sekta ya  Jua Kali. Kwa mujibu wa takwimu za serikali  asilimia 90 ya nafasi laki nane za ajira zilizobuniwa mwaka uliopita zilikuwa katika sekta hiyo.