array(0) { } Radio Maisha | Maraga ataka sheria ya dhulma za ngono kutathminiwa upya

Maraga ataka sheria ya dhulma za ngono kutathminiwa upya

Maraga ataka sheria ya dhulma za ngono kutathminiwa upya

Jaji Mkuu David Maraga ameendeleza shinikizo la kutaka  sheria ya dhulma za ngono kutathminiwa upya ili kuwalinda watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na minane ambao hushiriki ngono  kwa kusudi. Akizungumza katika warsha ya siku mbili kati ya Kenya na Uhispania, Maraga amerejelea kauli ambayo alitoa mwanzo akihojiwa ili kuchukua wadhfa huo ambapo alisema magareza ya humu nchini yamejaa watoto wa kiume ambao kosa tu lilikuwa kushiriki ngono na rika zao kwa hiari suala ambalo linaweza kushughulikiwa kwa njia nyingine.

Mwaka 2017 Maraga alirejelea suala hilo alipotembelea Gereza la Shimo la Tewa akisisitiza kwamba wanofaa kuadhibiwa chini ya sheria hizo ni watu wazima wanaoshiriki ngono na watoto.

Suala hilo lilirejelewa  mapema mwaka huu wakati ambapo majaji wa Mahakama ya Rufaa; Roselyn Nmabuye, Daniel Musinga na Patrick Kiage walipendekeza umri wa kushiriki ngono kwa hiari kupunguzwa hadi miaka 16. Walitoa ushauri huo wakati wa kumwachilia huru  kija mwenye umri wa miaka 15 ambaye alikuwa amefungw kwa kumtunga mimba msichana mwenye umri wa miaka 17.

Kwa mujibu wa sheria ya dhulama iliyowasilishwa bungeni na Jaji wa Mahakama ya Juu Njoki Ndung'u  mwaka 2006 akiwa mbunge maalum, yeyote anayeshiriki mapenzi na msichana mwenye umri chini ya miaka 11 anafaa kufungwa maisha, anayeshiriki na aliye katia miaka 12 na 15 miaka 20 na kati ya miaka 16 na 18 miaka 15.

Njoki anapinga vikali pendekezo la kupunguza umri wa hiari hadi miaka 16 japo majaji wengi wamekubalina na Jaji Mkuu David Maraga kuhusu haja ya kutafuta njia nyingine ya kushughulikia suala la waoto kushiriki mapenzi kwa hiari wenyewe kwa wenyewe kwani mara nyingi  wale wa kiume ndio hushtakiwa.