array(0) { } Radio Maisha | Tume ya EACC imewanasa maafisa 6 wa Mamlaka ya Mawasiliano

Tume ya EACC imewanasa maafisa 6 wa Mamlaka ya Mawasiliano

Tume ya EACC imewanasa maafisa 6 wa Mamlaka ya Mawasiliano

Maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabili  Ufisadi, EACC wamefanikiwa kuwakamata maafisa sita wakuu katika Mamlaka ya Mawasiliano wanaohusishwa na ukiukaji wa sheria za ununuzi. Maafisa hao ni Joyce NYambache ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi, wanachama wa Kamati ya Tenda, Stanley Kibe, Leo Kibet, Vincent Ngundi, Jane Jeptanui,  na Philip Kilpangat.

Aidha maafisa wafuatao wangali wanasakwa:

Mutua Muthusi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Wateja na Huduma za Umma, aliyekuwa mwanachama wa Kamati ya Tenda, Peris Nkonge na Katibu wa Mamlaka ya Mawasiliano, John Omo.

EACC imesema iliwasilisha fomu ya  uchunguzi wa maafisa hao kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, DPP  tarehe 16 mwezi Januari ambapo DPP alirejesha majibu kwa tume hiyo tarehe 6 mwezi huu akitoa idhini ya kukamatwa kwa washukiwa hao na kuwasilishwa mahakamani.