array(0) { } Radio Maisha | Serikali kuwakabili majambazi wa Matungu Kakamega

Serikali kuwakabili majambazi wa Matungu Kakamega

Serikali kuwakabili majambazi wa Matungu Kakamega

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dkt Fred Matiang'i ametangaza kuanzishwa kwa oparesheni maalumu kwenye eneo la Matungu, Kaunti ya Kakamega ili kuwakabili washukiwa wa uhalifu ambao wamekuwa wakitekeleza mauaji.

Akizungumza waakti wa ziara kwenye eneo hilo, Waziri Matiang'i amesema washukiwa kadhaa walikamatwa usiku wa kuamkia leo na wengine zaidi wanatarajiwa kukamatwa katika oparesheni ambayo itawajumuisha maafisa wa vitengo mbalimbali wakiwamo wale wa GSU.

Matiang'i ameilinganisha oparesheni itakayoendelezwa kwenye eneo hilo na ile iliyofanyika katika eneo la Mlima Elgon vilevile kuwakabili washukiwa ambao walikuwa wakitekeleza mauaji kiholela kukiwamo kuwabaka wanawake na watoto.

Waziri Matiang'i ameandamana na Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai kwenye ziara hiyo kwenye eneo la Magharibi ambako watu zaidi ya thelathini wameuliwa na kundi la wahalifu chini ya kipindi cha miezi miwili.

Uchunguzi wa awali umebainisha kwamba mauaji hayo yamekuwa yakitekelezwa na kundi la vijana kwa jina 42 Brothers, wanaofadhiliwa na baadhi ya wanasiasa ambao huwa wamejihami kwa panga na marungu na kinaya ni kwamba hawajakuwa wakiiba chochote kutoka kwa waathiriwa kabla ya kutoroka kwa kutumia pikipiki.