array(0) { } Radio Maisha | Sossio asema KNUT itaendelea kupinga Mtalaa Mpya wa Elimu

Sossio asema KNUT itaendelea kupinga Mtalaa Mpya wa Elimu

Sossio asema KNUT itaendelea kupinga Mtalaa Mpya wa Elimu

Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT, Wilson Sossion amesisitiza kuwa KNUT itaendelea kupinga utekelezaji wa mtalaa wa Umilisi, CBC hadi wakati Wizara ya Elimu itakapoweka mikakati ya kuboresha mtalaa huo.

Sossion amesema kulingana na mipangilio ya sekta ya elimu, kabla ya mtalaa mpya kuanzishwa ni lazima kuwe na vikao vya kuboresha na awamu ya kwanza ya majaribio hustahili kupewa mwaka mzima kabla ya kizinduliwa rasmi akitumia mfano wa mtalaa wa 8-4-4 ambao ulijaribiwa kwa miaka minne kabla ya kuzinduliwa rasmi.

Sossion aidha amesema kwamba majaribio ya mtalaa huo yalifanywa kwa wakati usiofaa bila kuwashirikisha washikadau wote.

Mwenyekiti wa KNUT Wycliff Emuchei amesema matamshi ya Waziri wa Elimu, George Magoha hapo Jana yalidhiirisha wazi mtalaa huo una dosari na wanafunzi hawastahili kufunzwa.