array(0) { } Radio Maisha | Kenya imechukua mkopo mwingine wa Bondi ya Yuro wa Shilingi Bilioni 210

Kenya imechukua mkopo mwingine wa Bondi ya Yuro wa Shilingi Bilioni 210

Kenya imechukua mkopo mwingine wa Bondi ya Yuro wa Shilingi Bilioni 210

Kiwango cha mkopo nchini kinatarajiwa kuongezeka baada ya Kenya kuchukua mkopo mwingine wa Bondi ya Yuro wa Shilingi Bilioni 210.

Shilingi bilioni 75 zitatumika kulipia bondi ya awali ambayo inatarajiwakulipiwa kufikia tarehe 24 mwezi Juni huku zilizosalia zikitarajiwa kupiga jeki miradi kadhaa ya ajenda nne kuu za serikali.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha, Henry Rotich, mkopo huo utalipwa kwa awamu mbili, mmoja ukiwa wa miaka saba na mwingine wa miaka 12. Ule wa miaka 7 utalipwa kwa riba ya asilimia 7 na ule wa miaka 12 kwa riba ya asilimia 8.

Hukuu utakuwa ni mkopo wa tatu kupitia  Bondi ya Yuro. Mara ya kwanza Kenya ilichukua mkopo wa shilingi bilioni 275 kisha bondi ya shilingi bilioni 200 kabla ya hii ya punde zaidi ya shilingi bilioni 210. Kwa jumla deni la Kenya kimataifa limefikia shilingi trilioni 5.5 huku  serikali ikiatarajiwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 550 kwa ulipaji wa mikopo katika bajeti ya mwaka 2019/2020.

Hali hii ya mikopo inaendelea kuibua wasiwasi miongoni mwa wakenya licha ya serikali kusisitiza fedha hizoz zinatumika.