array(0) { } Radio Maisha | Mshukiwa wa mauaji ya askari wa magereza kuzuiliwa kwa siku 14

Mshukiwa wa mauaji ya askari wa magereza kuzuiliwa kwa siku 14

Mshukiwa wa mauaji ya askari wa magereza kuzuiliwa kwa siku 14

Mahakama imelikubali ombi la maafisa wa polisi kuendelea kumzulia mshukiwa wa mauaji ya askari wa magereza, Peterson Njiru kwa siku 14 kukamiisha uchunguzi. Njru alikamatwa jana jioni kwa kuhusishwa na mauaji ya Pauline Wangari.

Inaarifiwa kuwa maafisa wa polisi walitumia picha zilizonaswa katika kamera za CCTV kumkamata mshukiwa, ambaye inadaiwa alionekana akiingia nyumbani kwa Wangari Jumatatu saa tatu usiku na kuondoka Jumanne saa tisa alfajiri.

Mwili wa marehemu ulipatikana nyumbani kwake, mtaani Kiharu Kaunti ya Murang'a ukiwa umeloa damu kwa kujeruhiwa.