array(0) { } Radio Maisha | Aliyekuwa Msemaji wa Serikali, Eric Kiraithe apewa majukumu mapya

Aliyekuwa Msemaji wa Serikali, Eric Kiraithe apewa majukumu mapya

Aliyekuwa Msemaji wa Serikali, Eric Kiraithe apewa majukumu mapya

Aliyekuwa Msemaji wa Serikali, Eric Kiraithe amepewa majukumu mapya katika Wizara ya Habari na Mawasiliano.

Kiraithe sasa atakuwa Katibu wa Utawala katika wizara hiyo baada ya nafasi aliyokuwa akishikilia kukabidhiwa aliyekuwa Msemaji wa Jeshi Kanali Mstaafu Cyrus Oguna. Kiraithe amemkabidhi rasmi ofisi hiyo muda mfupi uliopita katika ofisi hizo, Jumba la  Teleposta.

Haya yanajiri Oguna akitoa taarifa yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Msemaji wa Serikali na kukariri kuwa kwa sasa amestaafu katika jeshi na ni raia.