array(0) { } Radio Maisha | Bastola yapatikana ndani ya Choo Nairobi
Bastola yapatikana ndani ya Choo Nairobi

Maafisa wa polisi wamepata bastola aina ya Czeska na Risasi 15 ndani ya shimo la choo katika eneo la Mihang'o jijini Nairobi.

Kulingana na Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, DCI George Kinoti, bastola hiyo imepatikana ikiwa imefungwa kwa karatasi ya plastiki huku ikiaminika ilikuwa imehifadhiwa kwa takriban miezi miwili.

Hata hivyo uchunguzi unaendeela kufanywa ili kubaini iwapo iliibwa kutoka katika kituo cha Polisi cha Ruai..

Aidha kupitia mtandao wake wa Twitter, Kinoti amesema tayari mwanamke wa umri wa miaka 49 ambaye ni mmiliki wa choo ambacho bastola hiyo bandia imepatikana, amenaswa huku akihusishwa na wizi wa silaha katika eneo la Ruai mapema mwaka huu.

Kinoti amesema uchunguzi zaidi umeanzishwa ili kuwakamata washukiwa zaidi.