array(0) { } Radio Maisha | DCI yamnasa Mshukiwa wa uuzaji wa dhahabu bandia.

DCI yamnasa Mshukiwa wa uuzaji wa dhahabu bandia.

DCI yamnasa Mshukiwa wa uuzaji wa dhahabu bandia.

Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI wamemkamata Jared  Otieno, mshukiwa wa uuzaji wa dhahabu bandia katika msako unaoendelea. Aidha inaarifiwa kwamba magari yake mawili ya kifahari yamezuiliwa. Hayo yanajiri huku msako dhidi ya washukiwa wengine akiwamo Zaheer Jhanda wakitafutwa.

Ikumbukwe Jumanne Rais Uhuru Kenyatta kupokea malalamishi kutoka kwa Kiongozi wa Milki za Kiarabu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum akisema kwamba dhahabu zake zinazuiliwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta.

Tayari washukiwa kumi na watano wamefikishwa mahakamani huku maafisa wa polisi wakipewa wiki moja kukamilisha uchunguzi dhidi yao.