array(0) { } Radio Maisha | Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wafanyakazi, Jeremiah Kireini kuteketezwa

Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wafanyakazi, Jeremiah Kireini kuteketezwa

Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wafanyakazi, Jeremiah Kireini kuteketezwa

Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wafanyakazi, Jeremiah Kireini unatarajiwa kuteketezwa kuambatana na matakwa yake kabla ya kifo chake. Kiereini ambaye vilevile alihudumu katika nyadhfa mbalimbali serikalini na katika sekta ya binafsi aliaga dunia siku mbili zilizopita akiwa na umri wa miaka 90.

Kwa mujibu wa wandani wa familia yake, hafla ya heshima za mwisho itahudhuriwa tu na watu wachache.

Kiereini atakuwa  wa hivi punde zaidi miongoni mwa viongozi tajika ambao wamechagua kuteketezwa badala ya kuzikwa.

Mwaka uliopita, aliyekuwa mwanasiasa, Kenneth Matiba aliteketezwa kuambana na matakwa aliyokuwa ameweka wazi miaka 26 kabla ya kifo chake. Mwaka 2011, Mshindi wa Tuzo ya Nobel mwaka 2004  Wangari Maathai alitekekezwa katika makabauri ya Kariokor. Aliyekuwa Kanisa la Anglikana Manasses Kuria na mkewe Mary Kuria vilevile  waliteketezwa baada ya kufariki dunia.