array(0) { } Radio Maisha | NEMA yazifunga kampuni 25 zinazotupa taka katika Mto Nairobi

NEMA yazifunga kampuni 25 zinazotupa taka katika Mto Nairobi

NEMA yazifunga kampuni 25 zinazotupa taka katika Mto Nairobi

Mamlaka ya Kusimamia Mazingira, NEMA imezifunga kampuni 25 zinazoshtumiwa kutupa taka katika Mto Nairobi. 

Mkurugenzi wa NEMA, Geoffrey Wahungu amesema kampuni hizo zimekuwa zikielekeza taka kinyume na sheria katika mto huo licha ya kwamba juhudi za kuusafisha zinaendelea. 

Wahungu aidha amesema kampuni hizo ambazo hazijatimiza viwango vya utendakazi hali ambayo pia imechangia uamuzi wa kuzifunga.  

Kampuni ya Giloil ya kutengenza mafuta ya kupikia ni miongoni mwa zilizofungwa.