array(0) { } Radio Maisha | SRC yatishia kuzirejesha fedha ambazo wabunge wameidhinisha kuwa marupurupu ya nyumba

SRC yatishia kuzirejesha fedha ambazo wabunge wameidhinisha kuwa marupurupu ya nyumba

SRC yatishia kuzirejesha fedha ambazo wabunge wameidhinisha kuwa marupurupu ya nyumba

Tume ya Kuratibu Mishahara ya Wafanyakazi wa Umma, SRC imesema itazirejesha shilingi milioni 830 walizolipwa wabunge kwa marupurupu ya Nyumba.

Mwenyekiti wa SRC  Lyn Mengich amesema tume hiyo itachukua hatua za kisheria kwani malipo hayo yalifanywa kinyume na sheria. Amesema hakuna afisa yeyote wa serikali anayestahili kulipwa pesa zozote bila idhini ya SRC.

Ikumbukwe Tume ya Huduma za Bunge ilikuwa imeidhinisha malipo ya shilingi laki mbili unusu kwa kila mbunge kwa marupuupu ya nyumba hatua ambayo iliibua mjadala mkali nchini.

Mbali na marupurupu hayo wabunge hulipwa shilingi milioni ishirini za mkopo wa nyumba kumaanisha kwamba shilingi milioni mia moja hutolewa kwa gharama hiyo kila mwezi.