array(0) { } Radio Maisha | Maafisa wa KRA wanaoshtumiwa kuhusika ufisadi wapinga kuzuiliwa kwa siku 14

Maafisa wa KRA wanaoshtumiwa kuhusika ufisadi wapinga kuzuiliwa kwa siku 14

Maafisa wa KRA wanaoshtumiwa kuhusika ufisadi wapinga kuzuiliwa kwa siku 14

Maafisa thelathini na wanane wa Mamaka ya Ukusanyaji Kodi KRA,wamepinga uamuzi wa awali wa mahakama wa kutaka wazuiliwe kwa siku kumi na nne zaidi. Washukiwa hao wamewasilisha ombi katika mahakama Kuu kupinga uamuzi huo.

Siku ya Jumatatu, Mahakama Kuu iliamuru kuwa kumi na wannne hao wanastahili kuzuiliwa kwa wiki mbili korokoroni ili kutoa nafasi kwa maafisa wa upelelezi kufanya uchunguzi dhidi yao.

Hayo yanajiri huku maafisa wengine thalathini wa KRA wakifikishwa mahakamani leo hii, ambapo polisi wameiomba mahakama iwazuilie kwa siku ishirini na moja.

Kwingineko maafisa wanne wa mamlaka hiyo walioagizwa  kufika katika makao makuu ya Idara ya Upelezi DCI kuhojiwa,  wamewasilisha ombi wakitaka wasizuiliwe.