array(0) { } Radio Maisha | Mahakama ya Uajiri na Leba, imeondoa kosa la uhalifu dhidi ya viongozi wa Chama cha Wauguzi KNUN

Mahakama ya Uajiri na Leba, imeondoa kosa la uhalifu dhidi ya viongozi wa Chama cha Wauguzi KNUN

Mahakama ya Uajiri na Leba, imeondoa kosa la uhalifu dhidi ya viongozi wa Chama cha Wauguzi KNUN

Mahakama ya Uajiri na Leba, imeondoa kosa la uhalifu dhidi ya viongozi wa Chama cha Wauguzi KNUN. Jaji Byram Ongayo, amesema kesi dhidi ya Seth Panyako na viongozi wengine 10 haitaendelea hadi ombi la kupinga kesi hiyo litakaposikilizwa na kuamuliwa.

Chama  hicho kupitia wakili wake Edgar Busiega,  kimeiambia mahakama kwamba kesi ya uhalifu dhidi ya wateja wake haina msingi wowote kwani inahusu maswala ya wafanyakazi.

Wakili Busiega aidha amesema kuwashtaki wateja wake kwa kosa la uhalifu ni ukiukaji mkubwa wa sheria na  haki za viongozi hao wa KNUN. 

Panyako na wenzake walinaswa Octoba tarehe  29, mwaka wa  2018  wakituhumiwa  kusababisha usumbufu. Jaji Ongayo amesema kesi hiyo itasikilizwa Mei 20.