array(0) { } Radio Maisha | Makontena yenye madini ya Ethanol yanaswa jijiji Nairobi

Makontena yenye madini ya Ethanol yanaswa jijiji Nairobi

Makontena yenye madini ya Ethanol yanaswa jijiji Nairobi

Maafisa wa Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi, KRA wameyanasa makontena manne yenye madini ya Ethanol katika bohari moja jijini Nairobi, baada ya kupatikana yakiwa na mzigo tofauti na maelezo ya usafirishaji wake.

Makontena hayo yenye thamani ya shilingi takribani milioni 15, yamenaswa baada ya kubainika kuwa yalisafirishwa kutoka Uarabuni, kwa kisingizio cha kuwa mzigo wa chakula cha aina ya Spagheti  ili kukwepa kulipiwa ushuru.

Msimamizi wa kitengo cha Kudhibiti Uagizaji wa bidhaa Mipakani katika Mamlaka ya KRA, Kevin Safari, amesema maafisa wa mamlaka hiyo walikuwa kwenye oparesheni yao ya kawaida kabla ya kuyatambua makontena hayo yaliyokuwa na lita 57, 600 za madini ya Ethanol.

Safari amesema madini hayo yalikuwa yamefichwa baina ya pakiti 10, 600 za bidhaa za spagheti kwa lengo la kusafirisha madini yenyewe kisiri.

Tayari maafisa wa Upelelezi kwa ushirikiano na wale wa KRA wameanzisha uchunguzi wao ili kuwanasa waliohusika kwenye uhalifu huo huku wakiwalenga maafisa wa Mamlaka ya Bandari nchini KPA.