array(0) { } Radio Maisha | Polisi wawahakikishia usalama waumini wa Kiislamu wakati wa Ramadhan

Polisi wawahakikishia usalama waumini wa Kiislamu wakati wa Ramadhan

Polisi wawahakikishia usalama waumini wa Kiislamu wakati wa Ramadhan

Idara ya polisi imewahakikishia waumini wa dini ya kiislamu usalama msimu huu wa Ramadhan japo imewataka kuchukua tahadhari dhidi ya mashambulio.

Msemaji wa Polisi Charles Owino ameelezea kuwapo taarifa za kijasusi kwamba wanachama wa Al Shabab hupanga kutekeleza mashambulio kwa kuiga vita vilivyonakiliwa katika Quran katika Mtume Mohamed na Qureishi wa Makkah kwa kiingereza Battle of Badr.

Kadhalika amesema kundi hilo pia huenda likapanga mashambulizi ya kulipiza kisasi kufuatia kushambuliwa kwa msikiti Nchini New Zealand. Mwaka 2014, Kundi hilo lilitekeleza mauaji ya zaidi ya watu 150 katika Kaunti za Lamu na Tana River msimu wa Ramadhan.

Owino hata hivyo amesema kwasasa usalama umeimarishwa katika maeneo ya misikiti kadhalika kuwataka wenye taarifa zozote kuziripoti kwa polisi kutumia nambari ya dharura ya 999.