array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta aelekea Rwanda kwa ziara ya siku moja

Rais Kenyatta aelekea Rwanda kwa ziara ya siku moja

Rais Kenyatta aelekea Rwanda kwa ziara ya siku moja

Rais Uhuru Kenyatta ameondoka nchini kuelekea Rwanda kwa ziara ya siku moja.

Wakati wa ziara hiyo, Uhuru anatarajiwa kuwahutubua viongozi mbalimbali wa Bara Afrika watakaohudhuria kongamano la Transform Africa litakalofanyika jijini Kigali.

Kauli mbiu ya kongamano lenyewe ni 'Kupiga Jeki Uchumi wa Kidijitali Afrika' huku wageni zaidi ya elfu nne wakiratibiwa kujadili mada kadhaa kuhudu Masuala ya Teknolojia na Mawasiliano

Ziara hiyo inajiri siku moja tu baada ya Uhuru kukutana na Rais wa Ethiopia Sahle - Work Zewde katika Ikulu jijini Nairobi. Ziara hiyo ililenga kuboresha uhusiano kati ya Kenya na Ethiopia, kufuatia mvutano wa wafugaji ulioshuhudiwa hivi majuzi katika mpaka.