array(0) { } Radio Maisha | Magoha asema washikadau wa elimu watahamasishwa zaidi kuhusu mtalaa mpya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Magoha asema washikadau wa elimu watahamasishwa zaidi kuhusu mtalaa mpya

Magoha asema washikadau wa elimu watahamasishwa zaidi kuhusu mtalaa mpya

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema wizara yake itazindua mikutano ya washikadau kote nchini ili kuhamasisha umma kuhusu mtalaa unaoangazia milisi wa wanafunzi CBC.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwongozo kuhusu mtalaa huo mpya, Magoha amesema mikutano hiyo inalenga kuwafahamisha Wakenya kuhusu mfumo wa elimu, unaotumika nchini. Waziri Magoha amesema washikadau watakaoongoza mikutano hiyo ni maafisa wa Wizara yake, maafisa wa Tume ya Huduma za Walimu TSC, Wakuu Elimu kwenye Kaunti wale wa KICD miongoni mwa wengine.

Kilele cha mkutano huo, kitakuwa wakati wa kongamano la kitafa la elimu litakalofanyika Agposti mwaka huu.Wakati uo huo, Waziri huyo amewashtumu wale wanaopnga mipango ya kufanikisha kutekelezwa kwa mtalaa mpya wa elimu, akisema wamekuwa wakieneza taarifa  zizizo za kweli.

Aidha amesema kuna haja ya wizara yake pamoja na washikadau wengine kupewa muda kuutekeleza mtalaa huo kwani shughuli yenyewe inahitaji muda na si vyema kuishtumu hata kabla ya kufanikiwa.