array(0) { } Radio Maisha | Macharia Njeru aapishwa rasmi kuhudumu katika JSC

Macharia Njeru aapishwa rasmi kuhudumu katika JSC

Macharia Njeru aapishwa rasmi kuhudumu katika JSC

Macharia Njeru ameapishwa rasmi kuwa Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Nchini, LSK katika Tume ya Huduma za Mahakama, JSC.

Njeru ameapishwa mbele ya Jaji Mkuu, David Maraga katika majengo ya Mahakama Kuu, siku moja tu baada ya jina lake kuchapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali baada ya uchaguzi wenye ushindani mkali wa LSK.

Macharia ambaye awali alikuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kutathmini Utendakazi wa Polisi, IPOA sasa atakuwa mwanachama rasmi wa LSK na kuchukua nafasi ya Prof Tom Ojienda aliyekuwa akihudumu katika wadhifa huo baada ya kumshinda Ojienda katika uchaguzi huo.

Mwingine aliyeapishwa leo ni Jaji wa Mahakama Kuu, David Majanja ambaye sasa anajiunga na JSC ambako atawaakilisha majaji baada ya kutwaa wadhifa uliokuwa wa Jaji Aggrey Muchelule.