array(0) { } Radio Maisha | Mtoto aliyefariki dunia kwa kupewa dawa iliyozidi viwango kuzikwa Makueni
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mtoto aliyefariki dunia kwa kupewa dawa iliyozidi viwango kuzikwa Makueni

Mtoto aliyefariki dunia kwa kupewa dawa iliyozidi viwango kuzikwa Makueni

Mtoto wa miezi saba kwa jina Baby Ethan Muendo aliyefariki dunia kufuatia kudungwa sindano ya dawa ya Morphine katika hospitali ya Shalom Kaunti ya Machakos wiki iliyopita, atazikwa leo nyumbani kwa babaye Mukaa eneo la Kilungu Kaunti ya Makueni.

Ethan atazikwa huku uchunguzi kuhusu kifo chake ukiendelea kwani sampuli kutoka katika mwili wake zilipelekwa katika maabara ya kitaifa kuchunguzwa kiwango kamili cha sumu ya dawa hiyo iliyosabaisha kifo chake, matokeo ambayo bado yanasubiriwa, vilevile uchunguzi wa ubongo wake ukisubiriwa kufanywa tarehe 26 mwezi huu wa Mei, ili kutathmini kilichosababisha ubongo huo kuvimba.

Kesi dhidi ya washukiwa watatu ambao wamekuwa wahudumu katika hospitali hiyo inasubiriwa kuanza kusikilizwa huku washukiwa hao wakiendelea kuzuiliwa kwa kukosa fedha za kulipa bondi ya shilingi nusu million na mdhamini wa kiwango sawa na hicho, kila mmoja, hiyo ikiwa ni jumla ya shilingi milioni moja kwa kila mmoja.

Ikumbukwe kuwa hospitali hiyo ya Shalom ilifungwa wakati kisa hicho cha Baby Ethan kilipojitokeza, kikiwa ni kisa cha utepetevu ambacho kilisababisha Bodi ya Huduma za Matibabu nchini kuinyang'anya leseni ya kuhudumu, vilevile serikali ya Kaunti ya Machakos ikainyang'anya leseni ya biashara.

Kwa sasa, inasuburiwa kuona hatua itakayochukuliwa dhidi ya usimamizi wa hospitali hiyo akiwamo Mkurugenzi Mkuu, George Onyango ambaye alikamatwa pamoja na maafisa wengine, na ambao hawajafunguliwa mashtaka.