array(0) { } Radio Maisha | Mwilu ajiondoa katika kesi ambapo mfanyabiashara Geoffrey Asanyo analalamikia kubatilishwa kwa uamuzi wa kumfidia

Mwilu ajiondoa katika kesi ambapo mfanyabiashara Geoffrey Asanyo analalamikia kubatilishwa kwa uamuzi wa kumfidia

Mwilu ajiondoa katika kesi ambapo mfanyabiashara Geoffrey Asanyo analalamikia kubatilishwa kwa uamuzi wa kumfidia

Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu amejiondoa katika kesi ambapo mfanyabiashara Geoffrey Asanyo analalamikia kubatilishwa kwa uamuzi wa kumfidia shilingi milioni 43 baada ya kukamatwa kinyume na sheria mwaka 2002 na hata kushtakiwa.

Mwilu amesema sababu ya kujiondoa kwake ni kwa kuwa mmoja wa mawakili wa Asanyo, Okong'o Omogeni vilevile ni wakili wake katika kesi ya ufisadi inayomkabili hivyo hali hiyo inamnyima uhuru wa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Mfanyabiashara huyo alikuwa ameishtaki serikali kwa madai ya kumharibia sifa na kutatiza biahsara zake alipokamatwa mwaka 2002 kwa madai ya kumhonga aliyekuwa karani wa lililokuwa Baraza la Jiji la Nairobi, Zipporah Wandera kwa kumpa shilingi elfu mia moja themanini ili aipendelee mojawapo ya kampuni zake katika malipo.

 Hata hivyo mwaka 2009 Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliondoa mashtaka dhidi yake hali iliyomfanya kuwasilisha kesi kulalamikia kuharibiwa sifa. Mahakama ya Juu inatarajiwa kutoa uamuzi Mei 31 kuhusu kesi hiyo.