array(0) { } Radio Maisha | KVDA imetoa msaada wa chakula kwa watu zaidi ya 1, 000 Samburu

KVDA imetoa msaada wa chakula kwa watu zaidi ya 1, 000 Samburu

KVDA imetoa msaada wa chakula kwa watu zaidi ya 1, 000 Samburu

Mamlaka ya Maendeleo ya eneo la Kerio Valley KVDA imetoa msaada wa chakula kwa watu zaidi ya 1, 000 walioathiriwa na makali ya njaa katika Kaunti ya Samburu.

Mkurugenzi wa KVDA, Pauline Lenguris amesema mamlaka hiyo imeamua kutoa msaada huo unaogharimu shilingi laki tano kwa awamu mbili ili kuwanusuru watu wa maeneo hayo dhidi ya njaa na kwamba msaada huo utasambazwa hadi kwa wakazi waliotorokea misituni kufuatia kiangazi hasa kwa maeneo ya Samburu Mashariki.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Naibu Gavana, Julius Leseeto amesema mifugo vilevile wanahangaika kutokana na ukosefu wa malisho. Ikumbukwe serikali ya kaunti hiyo pia inanunua chakula japo kiwango chenyewe hakikidhi mahitaji ya wathiriwa.

KVDA imeweka mikakati ya kufanikisha upanzi wa miche katika eneo hilo ili kulinda misitu.