array(0) { } Radio Maisha | Viongozi waomboleza kifo cha Jeremiah Kiereini

Viongozi waomboleza kifo cha Jeremiah Kiereini

Viongozi waomboleza kifo cha Jeremiah Kiereini

Rais Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa waliotuma risala za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa wafanyakazi wa umma, Jeremiah Kiereini.

Kwa mujibu wa familia yake, Kiereini ameaga dunia akitibiwa katika hospitali moja hapa jijini Nairobi akiwa na miaka 90. Mbali na kuwa Mkuu wa Wafanyakazi Kiereini aliwahi kuhudumu katika Kampuni ya Kutengeneza Vileo ya EABL, Kampuni ya Mgarai ya CMC miongoni mwa nyingine.

Mbali na kusimamia kampuni kadhaa na kuhudumu serikalini, alikuwa mfanyabiashara shupavu huku akihusishwa na hisa katika kampuni kadhaa.