array(0) { } Radio Maisha | Kuleni Mamba ii kukabili maradhi- wapwani washauriwa

Kuleni Mamba ii kukabili maradhi- wapwani washauriwa

Kuleni Mamba ii kukabili maradhi- wapwani washauriwa

Huku takwimu ya Wizara ya Afya ya mwezi Septemba mwaka 2017 zikionesha kwamba asilimia 22.3 ya Wakenya wanaendelea kutibiwa maradhi ya shinikizo la damu, maambukizi ya maradhi hayo yanatarajiwa kupungua kwa asilimia kubwa endapo Wakenya watataanza kujitosa kwenye ulaji wa nyama ya Mamba.

Stephen Masha ambaye ni mfugaji wa Mamba kwenye Kaunti ya Mombasa anawashauri Wakenya kutoiogopa nyama hiyo anayoitaja pia kuyatibu maradhi mbalimbali yakiwamo ya pumu. Amedokeza kwamba kufikia sasa asilimia 30 pekee  ya Wakenya wanatumia kitoweo hicho.

Masha anazishinikiza Idara za serikali kuwaunga mkono wafugaji wa mnyama huyo ili kuwawezesha Wakenya kupata manufaa mbalimbali badala ya kuahangaisha mara kwa mara.

Wito wake unajiri huku ripoti hiyo ya Wizara ya Afya kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa shinikizo la damu ikibainisha kwamba asilimia nane ya wakenya wenye umri wa kati ya miaka 40 - 69 wako kwenye hatari ya aslimia 30 ama zaidi ya kuathiriwa na maradhi hayo.