array(0) { } Radio Maisha | Jina la Macharia Njeru lachapishwa rasmi katika Gazeti la Serikali

Jina la Macharia Njeru lachapishwa rasmi katika Gazeti la Serikali

Jina la Macharia Njeru lachapishwa rasmi katika Gazeti la Serikali

Jina la Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Nchini, LSK katika Tume ya Huduma za Mahakama, JSC, Macharia Njeru limechapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali. Hatua hiyo inafuatia uchaguzi wa wiki jana wa LSK vilevile kuteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Macharia Njeru sasa atakuwa mwanachama rasmi wa LSK na kuchukua nafasi ya Prof Tom Ojienda aliyekuwa akihudumu katika wadhifa huo.

Njeru alimshinda Ojienda katika uchaguzi huo baada ya Ojienda kupigania vikali kuruhusiwa kushiriki baada ya awali kuzuiliwa na Mamlaka ya Utozaji Kodi, KRA.

Kiongozi huyo alikuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kutathmini Utendakazi wa Polisi, IPOA.