array(0) { } Radio Maisha | Polisi Makueni waendesha uchunguzi kufuatia kifo cha ajuza

Polisi Makueni waendesha uchunguzi kufuatia kifo cha ajuza

Polisi Makueni waendesha uchunguzi kufuatia kifo cha ajuza

Maafisa wa polisi wa eneo la Kibwezi, Kaunti ya Makueni wanaendeleza uchunguzi kufuatia kifo cha ajuza wa umri wa miaka 83 aliyedungwa kisu shingoni na akafariki dunia akiendelea kutibiwa hospitalini.

Kwa mujibu wa Naibu Kamanda wa Polisi wa Kibwezi Geoffrey Nderitu, ajuza huyo alikuwa anaishi kwa nyumba ya mwanawe sokoni Kibwezi wakati kisa hicho kilitokea, na aliyepiga ripoti hiyo ni mkazamwana wake kuwa aliamka akapata mwanamke huyo amedungwa shingoni mnamo tarehe nane mwezi huu wa Mei mwaka huu.

Nderitu anasema huenda mshukiwa alikuwa ndani ya nyumba hiyo kwani milango ya nyumba hiyo haikuwa imevunjwa na pia wameweka ukuta uanozingira nyumba yote na hakuna ishara kuwa kuna mtu aliyeingia nyumbani.

Mwili wa mwanamke huyo umepelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Kibwezi ukisubiri kufayiwa upasuaji huku uchunguzi ukiendelea.