array(0) { } Radio Maisha | Aliyekuwa Rais wa Peru ajipiga risasi kabla ya kutiwa mbaroni

Aliyekuwa Rais wa Peru ajipiga risasi kabla ya kutiwa mbaroni

Aliyekuwa Rais wa Peru ajipiga risasi kabla ya kutiwa mbaroni

Aliyekuwa Rais wa Peru amejipiga risasi shingoni wakati polisi walipofika nyumbani kwake, kumkamata kufuatia tuhuma za ufisadi zinazomkabili. Alan Garcia, amepelekwa katika hospitali ya Casimiro Ulloa katika mji mkuu wa Lima kwa matibabu kufuatia tukio hilo.

Rais huyo wa zamani amekuwa akichunguzwa kwa tuhuma za ufisadi na ulanguzi wa pesa alipokuwa mamlkanani.

Taarifa nchini humo zinasema kuwa Garcia yuko katika hali mahututi.