array(0) { } Radio Maisha | Usafiri watatizika katika Uwanja wa JKIA kufuatia hofu ya kuwapo kwa bomu

Usafiri watatizika katika Uwanja wa JKIA kufuatia hofu ya kuwapo kwa bomu

Usafiri watatizika katika Uwanja wa JKIA kufuatia hofu ya kuwapo kwa bomu

Shughuli za usafiri zimetatizika kwa muda katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, JKIA baada ya kuibuka kwa hofu ya kuwapo kwa bomu katika ndege moja iliyokuwa ikisafiri kuelekea nchini Afrika Kusini.

Hofu hiyo ilizuka wakati mmoja wa abiria alipozozana na mhudumu mmoja katika ndege hiyo kisha abiria huyo kutaja neno bomb hali iliyoibua taharuki. Inaarifiwa kwamba abiria huyo tayari amekamatwa na kukabidhiwa maafisa wa  Kitengo cha Kukabili Ugaidi.

Aidha maafisa katika uwanja huo wamelazimika kuwakagua upya abiria na ndege uwanjani humo ili kuhakikisha hakuna hatari. Katika taarifa, Shirika la Ndege la Kenya Airways, KQ limesema limedhibiti hali kwa ushirikiano na idara za usalama.