array(0) { } Radio Maisha | Mahakama yasitisha kwa muda agizo la kuwatoza wafanyakazi 1.5%

Mahakama yasitisha kwa muda agizo la kuwatoza wafanyakazi 1.5%

Mahakama yasitisha kwa muda agizo la kuwatoza wafanyakazi 1.5%

Mahakama ya Uajiri na Leba imesitisha kwa muda agizo la serikali  la kuwaamrisha waajiri kuanza kuwakata wafanyakazi wao asilimia 1.5 ya mishahara ili kufanikisha ajenda ya serikali kujenga makazi ya bei nafuu. Katika uamuzi huo mahakama imeitaka serikali kuusitisha mpango huo hadi kesi iliyowasilishwa na  Muungano wa waajiri, itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Akiwahutubiwa wanahabari jijini Mombasa mapema leo Mkurugenzi Mkuu wa Muungano huo Jacqueline Mugo amesisitiza kwamba notisi iliyotolewa ni kinyume na sheria ikizingatiwa kwamba kesi inayohusu ada hiyo ingali mahakamani ikisubiri kusikilizwa ili kuamuliwa.