array(0) { } Radio Maisha | Mjadala wa marekebisho ya katiba wanoga katika kongamano la wawakilishi wadi Kisumu

Mjadala wa marekebisho ya katiba wanoga katika kongamano la wawakilishi wadi Kisumu

Mjadala wa marekebisho ya katiba wanoga katika kongamano la wawakilishi wadi Kisumu

Mjadala kuhusu iwapo kuna uwezekano wa kura ya maamuzi kuifanyia Katiba marekebsho itafanyika kabla ya uchaguzi mkuu kuandaliwa mwaka 2022, itafanyika, umetawala kongamano la wawakishi wadi linaloendelea mjini Kisumu.

Mbunge wa Rarieda, Otiende Amollo amesema ni wazi kuwa itakuwa vigumu kufanya baadhi ya mabadiliko kama vile kupunguzwa kwa idadi ya viongozi wa kisiasa wanaochaguliwa.

Hayo yanajiri huku seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior akisema kwamba huenda marekebisho katika Katiba yasiafikiwe kabla ya 2022, iwapo Jopokazi la upatanisho Building Bridges Initiative BBI lililobuniwa kufuatia maafikiano ya Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga halitaharakisha.

Seneta Mutula amesema kwamba, mgawanyiko unaoendelea kushughudiwa nchini miongoni mwa wanasiasa huenda ukalemaza Juhudi za jopo kazi hilo.

Amesema iwapo suala hilo litawasilishwa bungeni na kujadiliwa upo uwezekano kwaMa huenda wabunge wasiwe na msimamo mmoja kutokana na mgawanyiko huo.

Kuhusu suala la mgao wa fedha kwa serikali za kaunti, viongozi hao wamesisitiza kwamba, mgao huo unastahili kuongezwa. Sam Ongeri ni Seneta wa Kisii. Kongamano hilo lililoanza Jumatatu litakamilika leo hii.