array(0) { } Radio Maisha | Gavana Mutua aunga mkono marekebisho ya Katiba

Gavana Mutua aunga mkono marekebisho ya Katiba

Gavana Mutua aunga mkono marekebisho ya Katiba

Gavana wa Machakos Alfred Mutua, amesema kwamba migogoro ya kisiasa hasa baada ya uchaguzi itakomeshwa iwapo marekebisho yatafanyiwa Katiba ili kubuni nafasi zaidi za uongozi.

Akizungumza alipowasilisha mapendekezo ya Chama cha Maendeleo ChapChap mbele ya Jopo kazi la maridhiano BBI Jijini Nairobi, Mutua amesema ofisi ya upinzani inapaswa kupewa mamlaka zaidi sawa na ile ya Waziri Mkuu ili kuiwezesha kufuatilia utendakazi wa serikali.

Mutua ambaye ni Kinara wa chama hicho, amedokeza kwamba Kenya kwa sasa haina sera madhubuti kuukabili ufisadi na kwamba pana haja ya kubuniwa kwa sheria kali kuwakabili watu fisadi.

Wakati uo huo, chama hicho kimeitaka serikali kuhakikisha kinaanzisha kiwanda katika kila eneo bunge ili kubuni nafasi za ajira kwa vijana kukabili umaskini.

Jopo kazi la BBI chini ya uwenyekiti wa Seneta Yusuf Haji lilibuniwa baada ya maafikiano kati ya Rais Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga kuwapatanisha Wakenya.