array(0) { } Radio Maisha | Waziri Matiang'i asisitiza sheria inazingatiwa katika usajili wa watu kupitia mpango wa Huduma Namba

Waziri Matiang'i asisitiza sheria inazingatiwa katika usajili wa watu kupitia mpango wa Huduma Namba

Waziri Matiang'i asisitiza sheria inazingatiwa katika usajili wa watu kupitia mpango wa Huduma Namba

Mpango wa Huduma Namba umefuata taratiibu zote za kisheria - amesisitiza Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi kt Fred Matiang'i. Akizungumza muda mfupi uliopita katika kituo hiuki, Matiang'i amefafanua kwamba licha ya suala hii kuonekana kushika kasi mwaka huu limekuwa likijadiliwa na kutahminiwa kwa zaidi ya miaka miwili.

 Matiang'i amesisitiza kwamba kumekuwa na mashauriano ambayo yamewashusisha watu kutoak sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya uanahabari  kadhalika kujadiliwa bungeni.

Kuhusu iwapo wakenya wataendelea kupokea huduma, Mayiang'i amesema hakuna mkenya atakayenyimwa huduma kwa kukosa huduma namba japo itachukua muda zaidi ya inavyotakikana.

Hayo yakijiri, huku watu zaidi ya watu milioni 9 kote nchini wakiwa tayari wamesajiliwa kwa njia ya kidijitali, NIIMS vuguvugu la wakimbizi wanaoishi miongoni mwa wanajamii, National IDPs Network, limesema wanachama wake 8, 600 wamejipata kwenye njia panda wasijue wasajiliwe au la.

Wakati wa kikao na wanahabari kwenye makao makuu ya vuguvugu hilo mjini Kitale Kaunti ya Trans Nzoia, katibu mkuu Raphael Eyanai amesema walioathirika ni wale serikali iliwanunuliwa vipande vya ardhi na wanasubiri kugawanywa na kupewa hatimiliki hasa kwenye maeneo ya Nyandarua, Laikipia, Nakuru, Uasin Gishu na Trans Nzoia.