array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa pwani wamsuta Aisha Jumwa kwa kuingilia utendakazi wa Joho

Viongozi wa pwani wamsuta Aisha Jumwa kwa kuingilia utendakazi wa Joho

Viongozi wa pwani wamsuta Aisha Jumwa kwa kuingilia utendakazi wa Joho

 

Baadhi ya viongozi kwenye Kaunti ya Mombasa wameikosoa vikali hatua ya Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa kwa kuingilia utendakazi wa Gavana wa kaunti hiyo  Ali Hassan Joho.

Wakiongozwa na Mwakilishi wa Kike katika kaunti hiyo Aisha Mohamed, wamesema Gavana Joho anapaswa kuheshimiwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Likoni Mishi Mboko anahisi kwamba Jumwa amekosa kujiheshimu kufuatia matamshi ambayo amekuwa akiyatoa hasa anapokuwa kwenye majukwa mbalimbali.

Mishi amesema kwa namna moja Jumwa amefeli kama kiongozi ikizingatiwa kwamba anastahili kuwa mstari wa mbele katika kuzungumzia sera mbalimbali za kuwanufaisha wenyeji wa Pwani.

Ikumbukwe uhasama baina ya Joho na Jumwa ulianza baada ya Jumwa kufurushwa katika Chama cha ODM kufuatia hatua yake ya kutangaza kumuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Kulingana na Jumwa Joho alikuwa mstari wa mbele kushinikiza kufurushwa kwake chamani.