array(0) { } Radio Maisha | Usimamizi wa Nairobi Hospital umekana taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika hospitali hiyo.

Usimamizi wa Nairobi Hospital umekana taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika hospitali hiyo.

Hospitali hiyo imetoa taarifa baada ya kuenea kwa ripoti kwamba mfanyakazi mmoja amefariki dunia na wengine watano kulazwa hospitalini kufuatia mlipuko huo.

Hata hivyo imekiri kwamba wafanyakazi wake wanane ni miongoni mwa watu walioathiriwa na ugonjwa huo kufuatia mlipuko wa kipindupindu jijini Nairobi siku chache zilizopita na walitibiwa huku hospitali hiyo ikisema inaendelea kuwafuatilia kwa karibu wagonjwa waliolazwa hospitalini humo.

 Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa hospitali hiyo, Chris Abeid amesema kwa kipindi cha siku kumi zilizopita hospitali hiyo imewahudumia wagonjwa ishirini na watatu wa kipindupindu ambao walitibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.