array(0) { } Radio Maisha | Maseneta wameunga mkono pendekezo la awamu ya tatu ya mfumo wa ugavi wa raslimali kwenye serikali za Gatuzi

Maseneta wameunga mkono pendekezo la awamu ya tatu ya mfumo wa ugavi wa raslimali kwenye serikali za Gatuzi

Maseneta wameunga mkono pendekezo la awamu ya tatu ya mfumo wa ugavi wa raslimali kwenye serikali za Gatuzi

Maseneta  wameunga mkono  pendekezo la awamu ya tatu ya  mfumo wa ugavi wa raslimali kwenye serikali za Gatuzi

 

Maseneta  Moses Wetangula , Ledama Olekina, Sam Ongeri, Agnes Zani, Isaac Mwaura na profesa Margaret Kamar , wamesisitiza kuwa mfumo huo utaleta usawa na kuimarisha huduma msingi kwenye ugatuzi.

 

Seneta Olekina amedokeza kuwa mfumo huo utachangia pakubwa kwenye juhudi za kuthibiti ufisadi na utumiaji vibaya wa raslimali ya umma.

 

 

Kwa upande wake seneta wa Kisii Sam Ongeri,  ameapa kuwaleta pamoja maseneta kutoka Ukanda wa  Ziwa Victoria na maeneo mengine ili kuunga mkono mswada  unaohusu mfumo huo kwenye bunge la seneti.

 

Nalo kundi la  maseneta wa kike likiongozwa na Profesa Margret Kamar, wamesema kwamba  mpango huo unalenga kuboresha idara mbalimbali ambazo ni nguzo za ugatuzi.

 

 

Mfumo huo utapunguza mgao unaotengewa kaunti ambazo zimetengwa na kuongeza mgao kwenye kaunti ambazo zimeendelea kwa kipindi cha miaka mitano

   

 

Mwenyekiti wa  CRA  Jane Kiringai amesema mfumo huo umezingatia vigezi vipya vinavyohusisha   kilimo,afya ,elimu na elimu ya kiufundi

 

Ikumbukwe kwamba mfumo wa  awali wa ugavi wa raslimali ulitegemea idadi ya watu na viwango vya umaskini.