array(0) { } Radio Maisha | Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiangi ametetea hatua ya kuwapunguza walinzi wa baadhi ya wanasiasa wa Jubilee

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiangi ametetea hatua ya kuwapunguza walinzi wa baadhi ya wanasiasa wa Jubilee

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiangi ametetea hatua ya kuwapunguza walinzi wa baadhi ya wanasiasa wa Jubilee

Waziri wa  Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiangi ametetea hatua ya kuwapunguza walinzi wa baadhi ya wanasiasa wa Jubilee akisema kwamba shughuli ni yakawaida kwenye Huduma ya Kitaifa ya Polisi.


Kulindi la wanasiasa linalojiita Tangatanga ambalo limehusishwa na Naibu wa Rais  William Ruto, wameilaumu polisi kwa madai ya kutumia kuwanyamazisha kisiasa,kauli ambayo imepuuziliwa mbali na Matiang'i. Amewataka  wanasiasa kukomesha propaganda kwamba wanalengwa.


Ambao wameathirika na  hatua hiyo ya polisi ni pamoja na Gavana wa  Kiambu   Ferdinand Waititu, Seneta wa  Nakuru Susan Kihika, miongoni mwa wengine.


Matiangi amedokeza kwamba  mageuzi yanayoendelea kwenye idara ya polisi itawajumuisha polisi wa utawala kutoa ulinzi kwa wanasiasa. Kati ya polisi  100,000 ,  alfu kumi wanatoa ulinzi kwa  wanasiasa

Wakati uo huo, amesema kuwa risasi  13,000 na bunduki  700 zimerejeshwa kwenye shughuli ya kuwapiga msasa wamiliki wa  silaha inchin.