array(0) { } Radio Maisha | Wakenya wanakumbwa na uhaba wa dawa kutokana na deni la Shilingi bilioni 2.3
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakenya wanakumbwa na uhaba wa dawa kutokana na deni la Shilingi bilioni 2.3

Wakenya wanakumbwa na uhaba wa dawa kutokana na deni la Shilingi bilioni 2.3

Uhaba wa dawa unakisiwa kuendelea nchini, kufuatia deni la Shilingi bilioni 2.3 la Shirika la Kusambaza dawa KEMSA.

Kwenye ripoti iliyotolewa mwezi tarehe 11 mwezi huu,  ikijumuisha kaunti ambazo zimekwepa kulipia madeni hayo, Kaunti ya Nairobi inaongoza kwenye orodha ya aibu na kima cha shilingi  milioni 284 kuanzia mwaka wa 2014.  Uhaba wa dawa unazidi kuzikumba kaunti mbalimbali, licha ya serikali za ugatuzi kutenda mgao wa shilingi milioni 747 kufanikisha huduma za matibabu.

Dakatari Irene Muchoki ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu, amesema kwamba wakazi wa Nairobi watalazimika kutafuta huduma kwenye hospitali za  binafsi. Mapema mwaka uliopita , Waziri wa  Afya Sicily Kariuki alitoa makataa kwa serikali ya Nairobi kushughulikia uhaba huo na kuiamrisha KEMSA kuendelea kusamabaza dawa  licha ya deni la shilingi milioni 235.

Uhaba huo wa dawa umemfanya Gavana Mike Sonko kuwaachilia huru wagonjwa ambao walikuwa wamezuiliwa kwa kosa la kutolipia ada za matibabu.

Kando na Nairobi, Serikali zingine ambazo zinadaiwa na KEMSA  ni Homa Bay shilingi milioni 138 ,  Makueni shilingi milioni163,  Narok milioni 105,  Turkana  milioni 96 ,  Kiambu  milion 95 , Kitui  milioni 94, Nakuru  milioni 89 ,  Meru milion 88,   Vihiga  million 7 na  Wajir millioni 68.