array(0) { } Radio Maisha | Maafisa wa Idara ya Upelelezi leo hii wamefanikiwa kuwatia mbaroni washukiwa wanane wakiwa na fedha bandia

Maafisa wa Idara ya Upelelezi leo hii wamefanikiwa kuwatia mbaroni washukiwa wanane wakiwa na fedha bandia

Maafisa wa Idara ya Upelelezi leo hii wamefanikiwa kuwatia mbaroni washukiwa wanane wakiwa na fedha bandia

Maafisa wa Idara ya Upelelezi leo hii wamefanikiwa kuwatia mbaroni washukiwa wanane wakiwa na fedha bandia kwenye Mtaa wa Kiboko eneo la Lang'ata jijini Nairobi. Waliokamatwa ni  Wakenya wanne, raia mmoja wa Congo, wawili wa Tanzania na raia mmoja wa Nigeria. Raia hao wa Kenya wametambuliwa kuwa Boniface Mtwasi, Robert Riagah, Caleb Otieno na Michael Omondi.

Raia wa Tanzania waliokamatwa ni Manson Chogga na Konie Kalist. Aidha raia wa Congo ni  Ruhota Kabagale na Chukunosho Francis wa Nigeria.

Wamepatikana wakiwa na dola bandia za Marekani na kilo mia moja za dhahabu bandia. Washukiwa hao wamenaswa siku moja tu baada ya wengine sita kunaswa kwenye Mtaa wa Yaya Centre, jijini Nairobi wakiwa na dhahabu bandia.


Mwezi uliopita maafisa wa upelelezi vilevile walifanikiwa kuwanasa washukiwa kadhaa waliohusishwa na fedha zinazodaiwa kuwa bandia zilizopatikana katika Benki ya Barclays, Tawi la Queens Way, jijini Nairobi.